HISTORIA YA MWANAMAPINDUZI GUEVARA
WASIFU WAKE
Jina kamili: Ernesto Guevara
Kazi : Daktari, mwanamageuzi wa kijamaa (marxist)
Uraia : Argentina
Kuzaliwa : June 14, 1928
Kufariki : October 9, 1967
Mahali alipofikwa na
umauti : Bolivia katika milima ya La
heguera
Chanzo cha kifo
chake : kuuwawa kwa kupigwa risasi
MAISHA YAKE KWA
UJUMLA
Kama kijana msomi wa
shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la
Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona
maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko
mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo
kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.
Miaka ya
50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na
Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba
wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na
America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na
kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents) Punde tu baada ya
Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali
ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba
ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa
kilimo wa Cuba.
Mwaka
1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa
New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa
kukumbukwa” pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya
wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi)
alinukuliwa akisema “wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa
sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi,
serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya
Zaidi
inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu
hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?” MGOGORO WA CONGO – DRC
Miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida
“public life” na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja
gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya
wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo
ilishindikana na akakimbilia
Tanzania
na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku
akiishi kwa kujificha Baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro
na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za
America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama
mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa
ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta
Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores
KUKAMTWA
NA KUUWAWA
Mwaka 1967,
makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix
Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia,
asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo
yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa
kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake, Yasemekana
baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema “Usifyatue risasi, mi ni Che
Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa”
Alifungwa
kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya
raisi wa Bolivia ndugu kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati
huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili
hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja
kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya
kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga
risasi sita za kifua na kufa palepale Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake
haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho “Najua
umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume
kamili” .Aliacha wake wawili na watoto watano.
Makala hii
imeandaliwa na : Abraham Mndeme
Mwanafunzi chuo
kikuu cha Dodoma (UDOM)
Comments
Post a Comment