HISTORIA YA BENITO MUSSOLINI
Benito Amilcare Andrea
Mussolini (29 Julai 1883 – 28 Aprili 1945) alitawala Italia kidikteta kati ya 1922 hadi 1943.
Mwanasiasa wa
Kisoshialisti
Alisoma ualimu lakini alijiunga
na siasa na kuwa
mwanachama wa chama cha
kijamaa (soshialisti) cha Italia.
Akawa mhariri mkuu wa
gazeti la chama. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia alidai ya kwamba Italia
ijiunge na vita dhidi ya
Ujerumani akafukuzwa
katika chama kilichopinga
vita. Mussolini akawa
mwanajeshi. Mwanzo wa ufashisti Baada ya vita akatunga itikadi
yake ya ” ufashisti” akaunda harakati ya “Fasci di
Combattimento” (Muungano
ya mapambano). Wafuasi
wake mara nyingi waliwahi
kuwa wanajeshi wasioridhika
na matokeo ya vita na siasa ya nchi. Mussolini aliwavalisha
sare nyeusi na kuwapanga
katika vikosi kwa utaratibu
wa kijeshi. Idadi yao
iliendelea kukua haraka hadi
kufikia 200,000 mwaka 1922. “Mashati nyeusi”
walishambulia Wakomunisti
na Wasoshialisti na kuvunja
migomo ya wafanyakazi
wakipokea pesa kutoka
wenye viwanda au mashamba makubwa. Kwenye uchaguzi mkuu
mwaka 1921 Wafashisti
walipata wabunge 34.
Mussolini alibadilisha “fasci”
kuwa chama cha kifashisti cha
kitaifa (PNF). Wakati huohuo “mashati nyeusi” waliendela
kupigana na wafanyakazi na
wa soshialisti kwenye
barabara za Italia. Kiongozi wa serikali Hali ya vurugo ilisababisha
kuanguka au kujiuzulu kwa
serikali kadhaa. Mfalme
Vittorio Emanuele III
alioogopa vita ya ndani
akampatia Mussolini wito wa kuanzisha serikali mpya. 31
Oktoba 1922 Mussolini alikuwa
waziri mkuu wa Italia na
kiongozi wa serikali. Tangu mwaka 1924 aliimarisha
utawala wake. Kwa sheria
maalumu alibadilisha utaratibu
wa uchaguzi akajipatia
wabunge wengi. Sheria
zilizofuata zilipiga marufuku vyama vya upinzani.
Wanahabari wote walipaswa
kuwa wanachama wa chama
cha kifashisti. Hadi 1928
udikteta wa chama kimoja
ulisimama imara. Siasa ya nje Dikteta Mjerumani Adolf Hitler alikuwa amevutwa na siasa ya Mussolini akamwiga
katika mengi. Lakini Mussolini
hakumpenda Hitler hasa
itikadi yake ya kimbari.
Alikuwa na wasiwasi kuhusu
mipango ya Hitler dhidi ya Austria . Mwaka 1934 alituma wanajeshi mpakani na Austria
alipoogopa uvamizi wa
Wajerumani katika nchi ya
jirani. Katika siasa ya nje Mussolini
alikuwa na ndoto la kujenga
upya Dola la Roma la Kale. Mwaka 1935 alishambulia Ethiopia akitaka kujipatia koloni mpya na pia kulipiza
kisasi cha ushindi wa Ethiopia
dhidi ya Italia katika vita ya
Adua mwaka 1896. Italia ikafukuzwa katika Shirikisho
la Madola lakini ilifauli
kutawala Ethiopia yote. Katika Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Hispania tangu 1936 Mussolini alichukua upande wa jenerali Francisco
Franco. Kufukuzwa katika
Shirikisho la Madola na msaada
kwa Franco kulisababisha hali
ya karibu zaidi na Hitler. 25 Oktoba 1936 Mussolini na Hitler walitia sahihi mkataba wa
ushirikiano kati ya Italia na
Ujerumani. Benito Mussolini, Claretta Petacci na wengine walionyeshwa mbele ya
watu baada ya kuuawa. Vita Kuu ya Pili ya Dunia Albania Katika Aprili 1939 – kabla ya
mwanzo wa Vita Kuu – Italia ilivamia Albania. Jeshi la Italia ilipata matatizo makubwa
kushinda nchi hii ndogo.
Hivyo Mussolini alitulia
mwanzoni alipomwona Hitler
kushambulia Poland katika
Septemba 1939. Alikaa kimya pia Hitler alipovamia Ufaransa.
Mwishoni tu, siku chache
kabla ya ushindi wa
Ujerumani kukamilika,
Mussolini aliamua kuingia
katika vita akateka sehemu ndogo ya Ufaransa ya kusini. Ugiriki 28 Oktoba 1940 Mussolini
aliamrisha jeshi lake
kushambulia Ugiriki. Lakini Wagiriki walijitetea kwa
nguvu Waingereza wakawasaidia. Jeshi la
Wagiriki liliingia katika
Albania. Hitler alipaswa
kuingilia kati na kutuma
wanajeshi Wajerumani Ugiriki
waliofaulu kuwashinda Wagiriki na Waingereza
nchini. Afrika Mussolini alikuwa na
matumaini ya kwamba
ingekuwa rahisi kuvamia na
kuteka koloni za Uingereza
katika Afrika. Alipanga
kuwashambulia Waingereza kutoka koloni zake za Libya , Ethiopia na Somalia akilenga Misri, Somaliland ya Uingereza
na Kenya. Lakini mipango hii
ilishindikana. Mwisho Wakati huohuo Uingereza
ulizamisha manowari nyingi
za Kiitalia. Mwaka 1943
Waingereza na Waamerika –
waliowahi kuteka Afrika ya
Kaskazini- walivamia Italia ya kusini. Mussolini aliangushwa na
halmashauri ya chama chake
pamoja na mfalme akatupwa
katika jela. Wajerumani
walimwokoa gerezani lakini
hakuweza kutawala Italia tena. Alikuwa na eno ndogo
katika Italia ya Kaskazini. Katika siku za mwisho wa
vita kuu Mussolini alijaribu
kujiokoa mbele ya jeshi la
Waamerika waliokaribia kwa
kukimbia Uswisi. 27 Aprili
1945 Mussolini pamoja na wasaidizi wake na mpenzi
wake Clara Petacci
walikamatwa na
wanamgambo Waitalia
wakomunisti waliomwua
siku iliyofuata tar. 28.Ap
Comments
Post a Comment