HISTORIA YA MWANAMAPINDUZI GUEVARA
WASIFU WAKE Jina kamili : Ernesto Guevara Kazi : Daktari, mwanamageuzi wa kijamaa (marxist) Uraia : Argentina Kuzaliwa : June 14, 1928 Kufariki : October 9, 1967 Mahali alipofikwa na umauti : Bolivia katika milima ya La heguera Chanzo cha kifo chake : kuuwawa kwa kupigwa risasi MAISHA YAKE KWA UJUMLA Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America. Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fe...